Sunday, August 13, 2017

THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION

 (NACTE)

 TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU KUHAMA KWA OFISI YA NACTE KANDA YA KASKAZINI

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuuhabarisha Umma na wadau wa Elimu nchini hasa wa kanda ya Kaskazini ya kwamba, ofisi ya baraza ya kanda ya kaskazini imehamia katika jengo jipya la NSSF COMMERCIAL COMPLEX (MAFAO HOUSE) ghorofa ya nane (8), jengo hili lipo katika barabara ya Old Moshi, Plot No. 1. Karibu na New Arusha Hotel kuelekea Kibo Palace Hotel.

Kabla ya kuhama ofisi hizo zilikuwa katika majengo ya Arusha Technical College (ATC) Chumba namba nne (4), karibu na njia panda ya barabara ya kuelekea Nairobi (Namanga Road) na ile inayotoka Moshi.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Ofisi zetu za Kanda ya Kaskazini kwa anuani zifuatazo;-

NACTE Northern Zone
P.o. Box 14333 Arusha,
Mobile: 0658444556/57


IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI MAWASILIANO
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
3/08/2017

Tamko la HakiElimu juu ya Sera Mpya ya Elimu ya 2014

JOHN KALAGE MKURUGENZI MTENDAJI  HAKI ELIMU
Ndugu Wananchi; Itakumbukwa kwamba Februari 13, 2015 Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 ilizinduliwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Sera hii inaanza kutumika Mwaka huu (2016) wa masomo.
Sera hii, imefuta na kubatilisha matumizi ya sera nyingine za elimu zilizokuwa zikitumika kabla ya Mwaka 2015, zikiwamo Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996), Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa ElimuMsingi (2007).
Lengo la Sera hii, linatajwa kuwa ni kushughulikia changamoto za ki-elimu ambazo zinajitokeza zikiwemo udhaifu katika mfumo wa elimu na mafunzo, uhaba wa walimu, uhaba wa zana, nyenzo na vifaa na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na changamoto katika ithibati na udhibiti wa ubora wa shule na vyuo katika ujumla wake ambavyo vimechangia katika kushuka kwa ubora wa elimu na mafunzo nchini.
Ili kufanikisha lengo hilo, Sera imependekeza hatua mbalimbali ikiwamo kupunguza miaka ya kupata elimu kutoka 18 (2+7+4+2+3+) hadi 16 (1+6+4+2+3); Kiswahili na Kiingereza kuwa lugha za kufundishia katika ngazi zote, kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na kutoa ElimuMsingi bila Ada sambamba na kupunguza michango ya wazazi shuleni.
Ndugu Wananchi; tukiwa miongoni mwa wadau muhimu katika kuhakikisha maendeleo ya elimu nchini, HakiElimu kama shirika ambalo linataka kuona elimu nchini ikiwa bora, yenye usawa na yenye kuwajengea uwezo wahitimu kukabiliana na changamoto za kimaisha na ushindani katika soko, tumepitia tumetathmini malengo na mapendekezo yaliyomo ndani ya Sera hiyo, na tungependa kutoa maoni au msimamo wa shirika kuhusu Sera hii mpya kama ifuatavyo:
Kuhusu ubora wa elimu
Pamoja na kuwa malengo ya sera yanataja kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa nchini inakuwa bora na ya viwango vya ushindani, sera imeshindwa kufafanua ni jinsi gani itahakikisha kuwepo kwa ubora huo. Katika uchambuzi tumeonesha kuwa tafiti nyingi zinakubali kuwa ili elimu inayotolewa iwe yenye ubora ni lazima taifa lijitahidi kuboresha mazingira ya ufundishaji na kuwekeza katika ubora wa walimu ambao ndio msingi wa elimu yenyewe.
Hata hivyo Sera hii imekuwa kimya juu ya suala la ubora wa walimu na mazingira yao ya kuishi na kufanyia kazi. Sera haitamki suala la kuboresha maslahi ya mwalimu.
Aidha, ili kuhakikisha ubora mashuleni, shule, taasisi na vyuo vinapaswa kufanyiwa ukaguzi kuhusu ufundishaji, ujifunzaji, mazingira n.k. Hata hivyo sera hii haitoi mwongozo maalumu kuhusu namna ubora wa elimu utakavyo tathiminiwa na jinsi ya kuimarisha ukaguzi. Itakumbukwa kuwa Idara ya Ukaguzi kwa kipindi kirefu imekuwa ikikabiliwa na changamoto lukuki zikiwemo za uhaba wa bajeti na wataalamu. Takwimu zinaonesha kuwa hali ya ukaguzi nchini hairidhishi kwani ni takribani 40% tu ya taasisi za elimu ndizo hukaguliwa kwa mwaka..
Juu ya uwezo wa wahitimu kujiajiri,
Ndugu Wananchi lengo kubwa la mfumo wowote wa elimu duniani ni kuzalisha rasilimali watu. Pamoja na Sera hii mpya kuzungumzia kwa ujumla kuwa itaweka utaratibu utakaowawezesha wahitimu kuwa na uwezo wa kushindana katika soko la ajira pamoja na kujiajiri; haitoi mwongozo ni kwa namna gani au hasa ni nini kitafanyika ili kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa.
Changamoto kubwa ya zao la rasilimali watu linalozalishwa na shule na taasisi zetu imekuwa ni uwezo hafifu. Ushindani katika soko la ajira umeiweka pembeni Tanzania kiasi kwamba katika kushindania kazi za kimataifa tunashindwa kufua dafu hata mbele ya wenzetu wa Afrika Mashariki mathalani kutoka Kenya, Uganda na hata Rwanda. Ripoti ya World Economic Forum Network Readiness Index (2012 inaonesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya mwisho miongoni mwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki kwa kuwaandaa wananchi wake kuwa rasilimali watu yenye ujuzi na maarifa bora. Sera kama mwongozo ilipaswa kutoa utaratibu wa jinsi ya kulikabiri tatizo hili la uwezo wa wahitimu ili kuwezesha kuwa na ujuzi na maarifa yatakayowafanya waweze kuajiriwa na kujiajiri kirahisi zaidi.
Kuhusu lugha ya kufundishia
Ndugu Wananchi; Sera Mpya imeruhusu lugha za Kiswahili na Kiingereza kutumika kama lugha za kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini. Tamko hili la kisera si tu ni ishara ya Taifa kutokuwa na msimamo juu ya lugha ya kufundishia and kujifunzia, lakini pia sera haijabainisha malengo mahsusi ya kutumia lugha mbili kufundishia katika ngazi zote za elimu . Uchaguzi wa lugha ya kufundishia lazima ulenge kuwawezesha wanafunzi kufundishwa na kujifunza ipasavyo ili kupata ujuzi na maarifa tarajiwa. Pia uchaguzi wa lugha ya kufundishia lazima ulenge kuwawezesha wahitimu wa kada mbalimbali za utaalamu kuweza kushindana katika soko la kitaifa na kimataifa Tunaishauri serikali kutathmini utekelezaji wa agizo hili la kutumia lugha mbili ikizingatiwa mambo mawili (a) urahisi wa upatikanaji wa maarifa ya mjifunzaji yanayokidhi soko la ajira na mwingiliano wa kijamii kati ya nchi na nchi.
Suala la usawa katika utoaji elimu,
Ndugu Wananchii; Pamoja na kuwa sera imetamka kuwa itahakikisha usawa katika elimu inayotolewa, bado haikueleza ni kwa namna gani hilo linaweza kufanikiwa wakati bado shule za umma zinakabiliwa na changamoto nyingi za mazingira ya kujifunzia na kufundishia ukilinganisha na shule binafsi.
Wakati wanafunzi katika shule za umma wakikosa walimu bora kutokana na walimu kukimbia malipo duni na mazingira magumu, wakikosa vitabu na maabara, wenzao katika shule binafsi wananufaika na mazingira mazuri, hamasa ya walimu, uwepo wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na hivyo kuwawezesha kufanya wafaulu vizuri katika masomo yao kuliko wanafuzni wa shule za umma.
Kwa kushindwa kushughulikia suala hili, sera imeshindwa kupendekeza mbinu za kuondoa matabaka ya kielimu nchini ambayo yanawagawa watoto wa masikini kusoma kwenye shule zenye mazingira duni ya kufundishia na kujifunzia na watoto wa wenye uwezo kusoma katika shule zenye mazingira mazuri. Ikumbukwe kuwa wanafunzi walioko kwenye shule za umma ni asilimia 94.7 ya wanafunzi wote walioko elimumsingi kwa takwimu za mwaka wa 2015.
Rai yetu ni kuwa, ili kuleta usawa katika ujifunzaji ni lazima serikali ikishirikiana na wadau wa elimu iboreshe mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule za umma. Sera itoe mwongozo juu ya viwango maalumu vinavyohitajika kabla shule yeyote haijasajiliwa ili kuanza kutoa huduma elimu kama inavyofanya kwenye shule binafsi. Ni vyema pia viwango hivi vikahusisha kuwepo kwa miundombinu bora na ya kutosha vikiwamo nyumba za walimu, madarasa, vyoo, maji, maktaba, maabara na vifaa vyote muhimu vya kufundishia na kujifunzia.
Kuhusu ElimuMsingi bila Ada
Ndugu Wanahabari; Pamoja na kuwa wazo hili ni zuri na linaungwa mkono na wadau mbalimbali wa elimu ikiwamo HakiElimu, sera haikutoa utaratibu maalumu wa jinsi ambavyo tamko hili litafanikiwa. Serikali ni lazima ikumbuke kuwa kuwaweka shuleni watoto na wakajifunza ipasavyo kunahitaji gharama, tumeshuhudia utekelezaji wa sera ya elimu ya 1995 kupitia miradi ya MMEM na MMES ikishindwa kutokana uhaba wa bajeti.
Tayari serikali imeanza kutekeleza mpango wa kutoa elimu bila malipo kwa kuondoa ada na michango. Japo serikali imedhamiria kutoa 100% ya fedha za ruzuku kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa shule, bado kuna changamoto ya namna gani serikali itasaidia uboreshaji wa miundombinu shuleni ikizingatiwa kuwa shule hazipati fedha za shughuli za maendeleo na zimekuwa zikitatua matatizo ya miundombinu kwa kutumia michango ya wazazi. Tayari suala la elimu bila malipo limeanza kuleta mkanganyiko kwa wazazi na walimu wakuu hasa kuhusu uchangiaji wa kuboresha miundombinu ambao bado haujawekwa bayana na serikali. Serikali haina budi kuandaa mkakati utakaowezesha utekelezaji wa elimu bila malipo huku ikilenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katia shule zote za umma.
Ndugu Wanahabari; HakiElimu inapendekeza yafuatayo yawekwe kwenye miongozo ya utekelezaji wa Sera hii ili iweze kuleta tija na kusaidia kuboresha elimu yetu nchini.
Kama Taifa tunapaswa kutambua kuwa ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia unazifanya nchi na mataifa kuhusiana kwa karibu zaidi kuliko ilivyokuwa awali na hakuna taifa litakaloweza kuishi kama kisiwa. Ni muhimu Tanzania ikafanya tathmini hii na kuweka bayana msimamo wake kuhusu lugha tunayotaka kuitumia katika kuelimisha jamii na kizazi chetu kijacho. HakiElimu inaona kuwa njia pekee ya kutatua suala hili ni kuchagua lugha ambayo itaendana na uwekezaji ili kuwe na tija katika ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi ili wanafunzi wapate maarifa na ujuzi stahili na kuweza kushindana katika masoko ya ajira kimataifa
Suala la umri na miaka ya mwanafunzi kukaa shuleni lisipewe uzito kiasi cha kusahau jukumu la msingi la elimu nchini ambalo ni kuelimisha na kupandikiza weledi kwa watoto wetu. HakiElimu tunapendekeza badala ya kuweka uzito katika umri wa mwanafunzi, ni vema ikaangalia zaidi nini mwanafunzi anajifunza na vipi kinamsaidia katika kukabiliana na changamoto za kimaisha.
Kwa kuwa Sera bado inaruhusu taasisi binafsi na wadau kushiriki katika utoaji elimu nchini, ni muhimu pia ikaweka utaratibu maalumu wa jinsi ambavyo shule za umma zitaboreshwa ili kuondoa tofauti ya shule za umma na binafsi na hivyo kuondoa matabaka kielimu.
Ubora wa elimu umekuwa ni changamoto ya muda mrefu sasa na ni muda muafaka kwa serikali kuandaa mikakati itakayowezesha kuboresha elimu yetu katika ngazi zote za elimu. Njia pekee ya kufanikisha hili ni kuwa na shule bora za umma ambazo zinahudumia wanafunzi wengi, kuwa na walimu bora na wenye hamasa ya kufundisha, kuwa na mifumo ya kufuatilia na kutathmini kiwango cha elimu katika ngazi zote na mifumo bora ya usimamizi wa shule.
Mwisho tunaipongeza Serikali kwa juhudi za kuhakikisha Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 inapatikana.Hii ni baada ya kuwepo kilio cha muda mrefu kutoka kwa umma na wadau wa elimu kudai kufanyiwa marekebisho kwa sera za elimu za zamani ambazo ni dhahiri zilikwishapitwa na wakati na hivyo kushindwa kukabiliana na changamoto mpya za elimu.
Kupata nakala ya jarida lililobeba uchambuzi wa kina wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 tembelea http://www.hakielimu.org/publicatio...
Imetolewa na Idara ya Habari na Utetezi
HakiElimu
Mawasiliano: media@hakielimu.org

Friday, August 11, 2017


  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4

TEN/MET’s Meeting with Social Media stakeholders in Dar-es-salaam 2nd August 2017


TEN/MET's Meeting with Social Media stakeholders in Dar-es-salaam on 2nd August 2017 pic.twitter.com/UvbENNJ2Ou — Mtandao wa Elimu TZ (@ten_met) August 2, 2017 TEN/MET's Meeting with Social Media stakeholders in Dar-es-salaam 2nd August 2017https://t.co/5FLc3s9EHc pic.twitter.com/EBSl6Ksgut — Mtandao wa Elimu TZ (@ten_met) August 2, 2017 for more: https://khalfansaid.blogspot.com/search?updated-max=2017-08-02T04:18:00-07:00&max-results=7



Friday, August 11, 2017

Wakuu wa mikoa minne waanza kutekeleza agizo la Magufuli

By Burhani Yakub,Mwananchi byakub@mwananchi.co.tz



Kipindupindu chaanza kusambaa Mbeya




By Taboola

Ziara ya Waziri Mkuu Wilayani Chunya



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya SUNSHINE GROUP, Betty Mkwasa wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa Sunshine Mining Limited uliopo Chunya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Dennis Dillip ambaye ni Mjiolojia kuhusu mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni ya Sunshine Mining Limited uliopo Chunya wakati alipoutembelea Agosti 1, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakipata Maelezo kutoka kwa Afisa Madini wa Mkoa wa Mbeya Mhandisi Said Mkwawa kuhusu taarifa za Kampuni ya Sunshine Gold Mininga Limited wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni hiyo wilayani Chunya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia wimbo maalum unaozungumzia utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano ulioimbwa na Kwaya maarufu ya Kiwete katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Sabsaba mjini Chunya

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba  mjiini Chunya Agosti 1, 2017.  Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mkuki  kutoka kwa Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaso ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chifu wa makabila ya Wakimbu na Wasafa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia  kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Chunya Agosti 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2 MPANGO MKAKATI WA HAKIELIMU 2017 – 2021 (MUHTASARI)
Dondoo muhimu kuhusu HakiElimu
HakiElimu ilianzishwa mwaka 2001 na kundi la Watanzania 13 ambao waliweka nia thabiti na dhamira ya
dhati na ya muda mrefu kuleta mabadiliko kwenye elimu ya umma kwa watoto wote.
Dira
Kuwa na Tanzania yenye uwazi, haki na demokrasia ambapo watu wote wanafurahia haki ya kupata elimu
bora inayokuza usawa, ubunifu na kufikiri kiyakinifu.
Dhamira
Kuwawezesha watu kubadilisha elimu, ndani na nje ya shule; kushawishi utungaji wa sera na utekelezaji
wenye ufanisi; kuchochea mijadala bunifu ya umma na mabadiliko ya kijamii; kufanya tafiti, uchambuzi wa
sera na utetezi na kushirikiana na wadau ili kukuza ushiriki wa wananchi, uwajibikaji, uwazi na haki za kijamii.