Wednesday, March 30, 2016

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 Unashirikije Kuleta Maendeleo Kijijini Kwako
Utangulizi
Ushirikishaji Jamii ni jambo muhimu sana katika kufanikisha shughuli za maendeleo. Ushiriki na ushirikishaji
jamii unapaswa kuwa katika hatua zote za maendeleo ya mradi, yaani kuanzia kwenye kubuni mradi, kupanga
gharama na shughuli nzima ya utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji na tathimini ya mradi huo.
Miradi mingi ikiwemo ya elimu haifanikiwi kwa sababu tu ya kuwatenga na kutowashirikisha wananchi
katika mchakato mzima wa maamuzi ya uanzishaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi husika.
Lengo la kitabu hiki ni kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali ya kijamii, wakiwemo viongozi kuhusu
umu-himu wa kuwashirikisha wananchi katika michakato muhimu ya maamuzi kwa ajili ya maendeleo ya
jamii. Kwa upande mwingine, kitabu hiki kinalenga pia kuwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wao
kujihusisha na mambo ya msingi ambayo serikali au viongozi wao wanawaletea, iwe mitaani au vijijini
mwao. Kwa bahati mbaya wengi wao hawashiriki kikamilifu hata pale fursa zinapopatikana kwa kusingizia
kuwa na majukumu mengine hivyo kushindwa kushiriki katika miradi ya jamii ikiwemo ya shule. Aghalabu
hushindwa hata ku-washinikiza viongozi wao kuwashirikisha au kutekeleza miradi yao kwa mujibu wa
mipango mikakati. Matokeo yake ni kudumaa kwa miradi hiyo na maendeleo kwa jumla.
Nini Kifanyike kwa Viongozi na Wanajamii
Ni wazi, ushiriki au ushirikishaji wa wananchi katika michakato ya maamuzi, utekelezaji na usimamizi wa
miradi unachangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa huduma na uwajibikaji wa kila mdau kwa mradi husika.
Aidha, ushiriki na ushirikishwaji unaimarisha umiliki na usalama wa miradi ya jamii kwa kuwahusisha
wananchi wenyewe. Vilevile, ushiriki na ushirikishaji wa wananchi unachangia kwa kiasi kikubwa kuepusha
migogoro isiyo na tija ndani ya jamii

Friday, March 11, 2016

THE NGO

TWAWEZA yabaini Watanzania wana imani na mpango wa elimu bure.

Utafiti wa Taasisi ya Twaweza umebaini asilimia 88 ya Watanzania wanaimani na ahadi ya elimu bure kutekelezwa katika muda uliopangwa huku asilimia 76 wakiamini elimu hiyo kuwa na ubora zaidi.
Katika utafiti huo asilimia 15 wanaamini elimu bure haitaboresha elimu kutokana na ongezeko kubwa la uandikishwaji wa wanafunzi ambao utatumia rasilimali nyingi.
Matokeo hayo yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Mwanga Mpya kupitia takwimu zilizokusanywa kati ya Desemba 10, mwaka jana na Januari 2, mwaka huu kwa upande wa Tanzania Bara.
Pamoja na wananchi kuwa na imani na ahadi ya elimu bure wengi wamekuwa na mitazamo tofauti juu ubora wa elimu ya msingi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ambapo asilimia 49 wanasema ubora wa elimu umeongezeka na asilimia 36 wakibainisha kuwa elimu imezorota huku asilimia 14 wakisema hakuna mabadiliko yeyote.
Utafiti huo umebainisha kuwa wazazi wengi walikuwa wanaelemewa na michango ya shule ambapo wazazi na walezi 9 kati ya 10 huchangia elimu katika shule za umma.
Asilimia 89 ya wazazi wanakiri kulipa michango shuleni na asilimia 80 wakiripoti kulipa mpaka Sh50000 kwa mwaka huku asilimia 8 wakilipa zaidi ya Sh 100,000 kwa mwaka.
Utafiti huo pia umebainisha kuwa asilimia 37 ya wananchi wanaamini kuna uhusiano wa karibu kati ya jitihada za mwalimu na matokeo ya darasa la saba.
Mandhali katika chuo cha Maeneleo ya Wananchi Msaginya katika maeneo na matukio mbalimbali











TEACHERS: YOU ROCK THE WORLD