Tuesday, December 17, 2013

TUKISUBIRI KULETEWA HATUENDELEI KAMWE - tuelimike


by rahim kassonga
Elimu ndio uti wa mgongo wa taifa lolote lile duniani, lakini elimu ina misingi yake ipo mingi sana ila kwa leo nitasisitiza mambo mawili madogo ila muhimu sana.

Elimu bora na yenye manufaa hutolewa kuanzia utotoni, pia katika mazingira bora (conducive environment) hapa ndipo nilipoamua kusema tukisubiri mpaka serikali ije au wahisani watufikirie tutachelewa sana, tumeshachelewa sasa tutachelewa sana.

Tuelimike na tuchukue hatua sahihi na kwa umakini
tuelimike tusisubiri serikali au wahisani

Tusikubali vijana wetu wawe kwenye mazingira hatarishi kama haya
Watoto wanaweza kupoteza uhai kwa hali hii
Afya zao tunaziweka hatarini pia
Tunaweza kuwasababishia ulemavu usio wa lazima
Tukae kwa pamoja sisi wenyewe
Tujadili kwa kina
Tuchukue hatua
Hatimaye tuwajengee watoto wetu mazingira bora

Tukiamua kwa pamoja tunaweza
tuwajengee watoto mazingira bora kwani ndio tegemeo la taifa la baadae