Saturday, April 11, 2015

Tanzania ni Nchi yenye Amani na wananchi wake wamerithishwa Amani hiyo lakini jinsi siku zinavyosongambe ndivyo Amani yetu inazidi kuvurugwa na wachache tena tunaowategemea kuwa wamepevuka hasa katika masuala ya kielimu sasa hali inatisha hasa tunapoona wasomi wameona siasa ndiyo ukombozi wa maisha yao na si kwa manufaa ya wananchi na Nchi yao hebu wasomi wetu kuweni wazalendo kwa Nchi yenu siasa haitawapeleka popote. wewe kama msomi tumia uelewa wako kuikomboa Nchi kwa kutafsiri sera mbalimbali kwa manufaa ya Nchi na vizazi vya sasa na vijavyo





4 comments:

  1. mwelekeo wa elimu msingi bila malipo sasa wawa kivumbi kwa uandikishaji wanafunzi maana kila alifichwa atolewa ili aandikishwe lakini miundombinu sasa mmmmh

    ReplyDelete
  2. Riba za benki zawatesa wajasiriamali Shinyanga

    Baadhi ya wajasiriamali wadogo mkoani hapa wamesema riba kubwa zilizowekwa na baadhi ya taasisi

    Shinyanga. Baadhi ya wajasiriamali wadogo mkoani hapa wamesema riba kubwa zilizowekwa na baadhi ya taasisi za fedha zimekuwa zikichangia kushindwa kukopa.

    Wakizungumza kwenye mafunzo ya wajasiriamali wadogo yaliyolenga kuwapatia elimu kuhusu kufaidika na taasisi za fedha katika kukuza biashara zao, walisema riba kubwa ni kikwazo cha ustawi wao.

    Mshandete Mussa na Paulina Mashilingi, walisema kikwazo kinachowakabili ni uwapo wa riba hiyo, hivyo kushindwa kupata faida na kwamba, hatua ya benki kulegeza masharti itakuwa ni faraja kubwa kwao.

    “Tutaitumia vyema CRDB kukuza biashara zetu na kujiinua kiuchumi kutokana na masharti magumu kuondolewa na yaliyobaki yamelegezwa,” alisema Mashilingi.

    Meneja wa CRDB, Tawi la Shinyanga, Said Pamui alisema ulegezaji wa masharti unatokana na baadhi yao kushindwa kuitumia ipasavyo benki hiyo kukopa fedha ambazo zina riba nafuu, ili kupanua biashara na kufikia hadhi ya kimataifa.

    ReplyDelete
  3. MPANGO MKAKATI WA HAKIELIMU 2017 – 2021 (MUHTASARI) 1
    HAKIELIMU 2017 – 2021
    MPANGO MKAKATI WA
    HAKIELIMU (MUHTASARI)

    ReplyDelete
  4. HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
    Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na kutoa fursa ya kubadilishana uzoefu katika masuala yanayohusu elimu na Demokrasia kwa ujumla .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji
    wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0753 39 14 18 au 0784 98 18 89 au e-mail dmwaisaka@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

    ReplyDelete