1. TAARIFA ZA ASASI
Tuelimike
ni Asasi isiyo ya kiserikali inayofanyakazi Wilaya ya Mpanda Makao makuu yake
yapo Kijiji cha Isanjandugu, Kata ya Nsimbo Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi
imesajiliwa kwa namba 16NGO/00005237 chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya
kiserikali No. 24 ya mwaka 2002.
Tuelimike inalenga
kuiwezesha jamii kupata Elimu ndani na nje ya darasa ili kuweza kukuza
uelewa katika mazingira yanayotuzunguka
hasa maeneo ya vijijini kwani
Dira kugusa anga
za maarifa na kubadilishana uzoefu kujenga uwezo wa watu wa rika zote kama
kipaumbele cha kupata mabadiliko chanya.
Dhima kuangalia jamii vijijini kwa kutumia maarifa katika kuleta mabadiliko katika mipango ya kimaendeleo kwa kutumia fursa na maarifa kama njia ya kupunguza umaskini uliokithiri kwa kushirikiana, kujiamini na kithubutu.
2.
TAARIFA ZA WABIA WA MRADI
Mradi huu wa kilimo cha
umwagiliaji kwa njia ya matone ni mradi unaofadhiliwa na umoja wa Africa (AU)
kwa kushirikiana na Umoja wa Ujerumani
kupitia kitengo cha
AGYI_IF (African German Youth initiative- innovation
Fund) mradi huu unatekelezwa katika nchi tano za Afrika ambazo ni Tanzania,
Afrika kusini, Ghana, Togo na Benin.
3. TAARIFA ZA MRADI
Mradi
wa umwagiliaji kwa njia ya matone (Drip Irrigation) ni mradi unaotekelezwa na
Asasi ya Tuelimike katika Halmashauri ya Nsimbo hasa katika kata ya Nsimbo na
Uruwila.
Mradi
huu utaanzisha shamba darasa eneo la Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msaginya.
4.
MALENGO
Mradi
huu unalenga kuwawezesha vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 35 wakazi wa
Halmashauri ya Nsimbo ikiwa ni kuwataka wawe vijana wenye kujishughulisha
katika kujitafutia kipato kwa kutumia rasilimali ardhi iliyopo katika maeneo
yao.
Mradi
huu utawezesha vijana kuiga kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone.
5.
MAENEO/SHUGHULI ZA MRADI
Mradi
huu utajikita kuwezesha vijana kwenye kilimo cha mbogamboga kama vile kabeji,
pilipili hoho, nyanya na vitunguu maji kwa kutumia umwagiliaji wa matone.
6.
UTEKELEZAJI WA MRADI
Mradi
huu utatekelezwa kama ifuatavyo;
1. Kutoa
mafunzo kwa vijana kumi (10) watakao kuwa wawezeshaji kwa vijana wengine.
2. Kutoa
mafunzo ya ujasiliamali katika kilimo
3. Kutoa
mafunzo ya vitendo kwa vijana arobaini (40) kuhusu kilimo cha umwagiliaji na
namna ya kuandaa mifumo ya umwagiliaji
4. Kuunda
mtandao wa vijana wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji
5. Kuanzisha
shamba darasa la kilimo cha umwagiliaji
6. Kuwakutanisha
wakulima vijana na wadau ambao ni Taasisi za fedha, Wauzaji wa pembejeo za
kilimo na Wafanyabiashara watumiaji wa mazao ya bustani.
Mawasiliano
Asasi ya Tuelimike
S. L. P 200, Mpanda -Katavi,
Simu:+255753391418/+255784981889
Email:twelimike@gmail.com